Home kimataifa AUBA AAMBIWA MAKALI YAKE YAMEPUNGUA

AUBA AAMBIWA MAKALI YAKE YAMEPUNGUA


MCHAMBUZI wa masuala ya michezo, Jamie Redknapp amesema kuwa mshambuliaji wa kikosi cha Arsenal, Pierre Emerick Aubameyang anaonekana kupoteza yale makali yake ya zamani kwa msimu huu wa 2020/21.

Wakati Arsenal ikipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Manchester City kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa Uwanja wa Emirates, safu ya ushambuliaji ya Arsenal ilionekana kuwa butu ndani ya uwanja.

Takwimu zinaonyesha kuwa Arsenal walipiga jumla ya mashuti 7 na katika hayo ni moja lililenga lango huku City wakipiga jumla ya mashuti 15 na matatu yalilenga lango jambo ambalo limempa nguvu mchambuzi huyo kuweka wazi kwamba kuna kazi kwa Arsenal ya kufanya katika safu ya ushambuliaji.

Bao pekee la Manchester City inayonolewa na Pep Guardiola lilipachikwa dakika ya  2 na Raheem Streling na lilidumu mpaka mwisho wa mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa kutoka kwa vijana wa Mikel Arteta.

Raia huyo wa Gabon msimu uliopita aliweza kufunga jumla ya mabao 29 kwenye mashindano yote aliyoshiriki ila msimu huu mambo kwake yamekuwa magumu kwa kuwa hajajenga ushkaji na nyavu.

Matokeo hayo yanaifanya Arsenal kubaki na pointi zao 34 ikiwa nafasi ya 10 huku City ikijikita kileleni na pointi zake ni 59.

“Ninaona kwamba kuna nguvu ambayo ameikosa msimu huu tofauti na awali hivyo kuna kazi kwa Auba ya kufanya ili kurejea kwenye makali yake ndani ya uwanja,” amesema.

SOMA NA HII  WAKATI LEO DUNIA NZIMA IKITAZAMA QATAR...MERIDIANBET WANAKUPA MCHONGO HUU...ZINGATIA HAYA TU...