Home Uncategorized MAYANJA ATAJA SABABU ZA KUTUA KMC, ATAJA ATAKAOWASAJILI

MAYANJA ATAJA SABABU ZA KUTUA KMC, ATAJA ATAKAOWASAJILI

KOCHA mpya wa KMC, Jackson Mayanja amesema kuwa sababu kubwa iliyomfanya akubali kusaini klabu ya Halmashauri ya Kinondoni, KMC  ni mfumo wa klabu hiyo kumvutia na ubora wa kikosi.

Mayanja leo amesaini kandarasi ya mwaka mmoja kukinoa kikosi hicho ambacho kilikuwa chini ya Etiene Ndayiragije ambaye kwa sasa yupo Azam FC.

“Nimekubali kusaini KMC kwa kuwa ni klabu yenye mfumo mzuri wa uendeshaji hivyo nina imani tutafanya vema kwenye ushindani.

“Sina mpango wa kuja na wachezaji wangu ila ikipendeza nitakuja na mtu wa benchi la ufundi ili tusaidiane kwenye majukumu,” amesema.

SOMA NA HII  ALLIANCE FC WAIPIGIA HESABU NDEFU NAMUNGO