Home news KISA MKWANJA…YANGA WAACHANA NA CHICO…NABI ASHINDWA KUJIZUIA..’ABUBUJIKWA’ NA HAYA….

KISA MKWANJA…YANGA WAACHANA NA CHICO…NABI ASHINDWA KUJIZUIA..’ABUBUJIKWA’ NA HAYA….


KOCHA wa Yanga, Nasreddine Nabi ametoa sababu ya kufa kwa dili la winga kutoka TP Mazembe, Chico Ushindi kwamba dau lake, lilikuwa linaweza likasajili mastaa wengi wa kiwango cha Fiston Mayele.

Nabi alisema anakubaliana na kiwango cha Ushindi ila gharama yake si ya kitoto na analiona ni jambo ambalo litaondoa usawa kwa wachezaji.

β€œGharama yake kumchukua kwa mkopo wa mwaka mmoja unaweza ukawasajili mastaa wengi kama Mayele, sasa sijaona sababu ya kumchukua, pia naepusha migogoro ya wachezaji wengi kuanza kujiuliza mbona huyu ana gharama kubwa,” alisema bila ya kutaja pesa ambayo ingewagharimu Yanga ili kumpata Ushindi kwa mkopo.

Wakati Nabi, ananyoosha mikono juu kuhusu staa huyo, kwa upande wa mchezaji huyo anaonekana bado kuwa na matumaini na viongozi wa Yanga kwamba watafanya jambo.

Ushindi alisema muda wote ambao anasubiri kuna ukimya mkubwa kutoka kwa meneja wa Kikongo ambaye alimfahamisha kuhusu dili hilo, lakini yeye yupo tayari kuja kucheza Yanga iwapo tu mabosi wa pande zote mbili watakubaliana.

β€œYanga wanatakiwa wazungumze na Mazembe kama wananihitaji mimi, niko tayari kuja na kama ningekuwa na jibu kutoka huko basi ningejua nazungumzaje na timu yangu, barua rasmi pia ifike kwa mabosi zangu,” alisema Ushindi.

SOMA NA HII  ROBERTINHO ATAMBA KUHUSU KIKOSI CHA SIMBA