Home Uncategorized AZAM FC WAJANJA KINOMA, WAITIBULIA SIMBA KWA MSHAMBULIAJI HUYU MATATA

AZAM FC WAJANJA KINOMA, WAITIBULIA SIMBA KWA MSHAMBULIAJI HUYU MATATA


MSHAMBULIAJI wa Azam FC Andrew Simchimba amejifunga ndani ya klabu hiyo kwa kandarasi ya miaka mitatu.

Nyota huyo inaelezwa kuwa alikuwa kwenye hesabu za mabosi wa Kariakoo, Simba waliokuwa wanahitaji kuipata saini yake kwenye dirisha dogo hivyo dili lao limeshatibuka.

Simchimba aliyekuwa anakipiga Coastal Union kwa mkopo na sasa amerejea Azam FC mkatba wake ulikuwa unameguka mwezi Septemba mwaka huu na kuongezewa kandarasi yake ya miaka mitatu atadumu hapo kwa miaka mitatu mpaka 2023.

Benchi la ufundi la Azam FC limekuwa likimwamini nyota huyo ambaye amekuwa akitimiza majukumu yake kwenye timu hiyo ya Azam FC.

Kwenye sare ya kufungana bao 1-1 na Ndanda FC alifunga bao la kufutia machozi kwa timu yake na kuipa pointi moja ilipokuwa kwenye ziara ya nyanda za juu Kusini.

SOMA NA HII  MECHI TANO ZA MWANZO KWA YANGA KUNAKO LIGI KUU BARA, WAMO COASTAL UNION