Home Uncategorized YANGA YAITANGAZIA VITA JUMLAJUMLA SIMBA, MACHI 8 TAIFA

YANGA YAITANGAZIA VITA JUMLAJUMLA SIMBA, MACHI 8 TAIFA

UONGOZI wa  Yanga umesema kuwa utaonyesha soka safi lisilo na makandokando kwenye mchezo wao utakaochezwa Machi 8, Uwanja wa Taifa dhidi ya Simba.

Yanga iliyo chini ya Luc Eymael itakutana na Simba kwenye mchezo wa pili wa Ligi Kuu Bara ikiwa na kumbukumbu ya kutoka sare ya kufungana mabao 2-2 Januari 4.

Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema:” Mashabiki wa Yanga ni siku yetu kuonyesha soka lisilo na makandokando na kila mchezaji anajua jukumu lake tupo tayari kuonyesha soka safi kwa kuwa tumejipanga na tunaamini inawekezakana.

“Kwenye mchezo wetu dhidi ya Simba tuna kazi moja ya kutafuta ushindi ukizingatia kwamba tumetoka kumalizana na Mbao na kupata ushindi mnono wa mabao 2-0,”.

SOMA NA HII  YANGA YAINGIA ANGA ZA KIUNGO HUYU RASTA FUNDI