Home Uncategorized YANGA YAINGIA ANGA ZA KIUNGO HUYU RASTA FUNDI

YANGA YAINGIA ANGA ZA KIUNGO HUYU RASTA FUNDI


INAELEZWA kuwa Klabu ya Yanga ipo katika mpango wa kuinasa saini ya kiungo wa Kagera Sugar, Awesu Awesu ambaye amekuwa kwenye kiwango kizuri kwa msimu wa 2019/20.

Taarifa zinaeleza kuwa mkataba wa Awesu na Kagera Sugar unamalizika mwisho wa msimu huu hivyo Yanga itamsajili mchezaji huyo akiwa huru.

“Kwa sasa Yanga inahitaji kuboresha kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao wa 2020/21 baada ya kushindwa kufanya vizuri msimu huu, hesabu kubwa ni kutofanya makosa tena hivyo Awesu ameonekana kuwa chaguo la kwanza la kocha,” ilieleza taarifa hiyo.


Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael anatajwa kuongeza nguvu kusaka saini ya nyota huyo kwa kuwa alivutiwa na uwezo wake walipokutana kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho, Uwanja wa Taifa.

Nyota huyo mwenye rasta kichwani alifunga bao pekee kwa Kagera Sugar kwenye mchezo huo ambapo walipoteza kwa kufungwa mabao 2-1.

Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa ni suala la kuwa na subira kwani kwa sasa dirisha la usajili bado halijafunguliwa.

SOMA NA HII  CHAMA AFUNGUKIA ISHU YA MKATABA WAKE SIMBA KISA YANGA