Home Uncategorized SIMBA: TUMEFUNGA HESABU KISHUJAA AFRIKA KUSINI

SIMBA: TUMEFUNGA HESABU KISHUJAA AFRIKA KUSINI


PATRICK Aussems, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa uwezo wa wachezaji wake umeimarika hivyo ana imani kubwa watakuwa na kitu cha kipekee msimu ujao.

Simba jana ilifunga hesabu nchini Afrika Kusini kwa kutoka sare ya kufungana bao 1-1 na Orlando Pirates mchezo wa kirafiki uliochezwa Afrika Kusini.

Aussemss amesema:-“Tumemaliza kambi na Orlando Pirates ambao wapo tayari kuliko sisi wao wametumia muda mwingi kujiaandaa kwa ajili ya msimu ujao tofauti na sisi.

“Napenda kuwapongeza wachezaji wangu tulikuwa na wakati mzuri sana Rustenburg, kila mmoja kafanya kazi nzuri tunaweza kusema hii kambi imekuwa nzuri sana na nimeridhishwa kwa hatua ambayo tumefika,” amesema.

SOMA NA HII  BABA MANARA AFUNGUKA USAJILI WA YANGA, MASHABIKI WA YANGA NI WENGI