Home Habari za michezo BAADA YA KUWAONA YANGA NA TAMASHA LAO…PITSO MOSIMANE KATIKISA KICHWAA WEE..KISHA AKASEMA...

BAADA YA KUWAONA YANGA NA TAMASHA LAO…PITSO MOSIMANE KATIKISA KICHWAA WEE..KISHA AKASEMA HAYA…


Kocha mwenye ‘Profile’ Pitso Mosimane raia wa Afrika ya Kusini amekiri kuwa Yanga ni miongoni mwa vilabu vikubwa barani Afrika.

Pitso ameyasema hayo muda mchache baada ya kutamatika kwa Tamasha kubwa la Klabu ya Yanga linalojulikana kama ‘Siku ya Mwananchi’ ambalo alialikwa kushiriki kilele cha Tamasha hilo.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Pitso ameandika;

“Nimetembea takriban 70% ya bara la Afrika, kwa mtazamo wangu, Yanga ni miongoni mwa timu kubwa Afrika”

Kauli hiyo ya Pitso inakuja miezi michache tangu alipoeleza kushangazwa kwake na mwamko wa Mashabiki wa vilabu vya Tanzania baada ya kushuhudia gwaride la Ubingwa wa Ligi Kuu lililofanywa na Yanga, ambalo juzi alikiri kuwa lilipeleka ujumbe duniani.

Pitso alikuwepo jukwaani wakati Yanga ikipoteza kwa magoli 2-0 mbele ya Mabingwa wa Uganda Vipers SC katika kilele cha maadhimisho ya ‘Siku ya Mwananchi’

Pitso Mosimane amewahi kuvifundisha vilabu vya Mamelodi Sundowns na Al-Ahly huku kote akifanikiwa kubeba taji la Ligi ya Mabingwa Afrika.

SOMA NA HII  KUHUSU ISHU YA MASHABIKI KUSHINDWA KUANGALIA MECHI RWANDA, UONGOZI WA YANGA WASEMA HAYA