Home Simba SC SIMBA: AL MERRIKH HATOKI KWA MKAPA

SIMBA: AL MERRIKH HATOKI KWA MKAPA


 HAJI Manara, Ofisa Habari wa Simba amesema kuwa kwa namna ambavyo kikosi kimejipanga licha ya kwamba watakosa huduma ya mchezaji wao namba 12 wana imani wataibuka na ushindi mbele ya Al Merrikh.

Simba itamenyana na Al Merrikh, Machi 16, Uwanja wa Mkapa ikiwa ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa hatua ya makundi. Mchezaji wao namba 12 ambaye ni shabaki amezuiwa kuingia na Shirikisho la Soka Afrika, (Caf).

Manara amesema kuwa wanatambua kwamba umuhimu wa mashabiki ndani ya uwanja ni mkubwa ila itakuwa ngumu kwa Wasudan hao kutoka salama Uwanja wa Mkapa.

“Naamini kwamba kwa namna wachezaji ambavyo wamejipanga na maandalizi ambayo yanaendelea itakuwa ngumu kwa Wasudan kutoka salama kwa Mkapa.

“Pale alikuja Al Ahly tulimshinda, alikuja AS Vita tulimpiga sasa ni zamu ya Al Merrikh na maombi yetu na imani yetu ni kupata ushindi hakuna jambo jingine.

“Tutacheza bila mashabiki haina tatizo licha ya kwamba mashabiki ni mastaa wetu namba moja na wamekuwa nasi kila hatua hakuna namna haya ni masuala ya mamlaka huwezi kupingana nayo.

“Lakini tukija kwenye uhalisia tunahitaji pointi tatu, kwa Mkapa tuna pointi zetu 9 ambazo tunazihitaji tayari tumechukua tatu hivyo bado kazi inaendelea,” amesema.  

Kwenye kundi A, Simba inaongoza ikiwa na pointi 7 inakutana na Al Merrikh ambayo ina pointi moja kibindoni. Wapinzani wao tayari wameshatua timu Bongo kwa ajili ya maandalizi ya mwisho.


SOMA NA HII  SKUDU NA SIMBA MPAKA KIELEWEKE