Home Yanga SC MWL KASHASHA :- MUANGOLA WA YANGA BADO HAWEZI KUCHEZA LIGI YA BONGO

MWL KASHASHA :- MUANGOLA WA YANGA BADO HAWEZI KUCHEZA LIGI YA BONGO


  
MCHAMBUZI wa masuala ya michezo Bongo, Mwalimu Alex Kashasha amesema kuwa anaona wazi kwamba kiungo mshambuliaji wa Yanga, Carlos Carlinhos hawezi kucheza ndani ya kikosi hicho kutokana na kasi ya Ligi Kuu Bara.


Carlinhos, raia wa Angola ni ingizo jipya ndani ya kikosi hicho ambacho kipo chini ya Kaimu Kocha, Juma Mwambusi baada ya Cedric Kaze kufutwa kazi, Machi 7.

Kwa sasa Yanga ipo kwenye mchakato wa kusaka kocha mpya ambapo imeweka wazi kwamba imepata zaidi ya CV 72.

Kashasha amesema:-”Naona kwamba bado Carlinhos hajawa na ile nguvu ya kucheza ndani ya Yanga kwa sababu mpira ule wa kugonganagongana ndani ya uwanja anaonekana hauwezi, yaani ni aina ya wachezaji ambao hawataki shida jambo ambalo halipo kwenye ligi yetu,” .

Ndani ya ligi Muangola huyo amecheza jumla ya mechi sita na amehusika kwenye jumla ya mabao matatu na ana pasi mbili za mabao kati ya 36 yalifungwa na timu hiyo.

SOMA NA HII  KAMPUNI 10 ZA KIMATAIFA ZAJITOKEZA KUUJENGA UWANJA WA YANGA KIGAMBONI