Home Habari za michezo SKUDU NA SIMBA MPAKA KIELEWEKE

SKUDU NA SIMBA MPAKA KIELEWEKE

Habari za Simba leo

WAKATI kikosi cha Yanga kikianza ratiba ngumu ya maandalizi baada ya kukamilika winga mpya wa timu hiyo Mahlatse Makudebela maarufu Skudu, amesema anataka kuwaona Simba ili afahamu ubora wao.

Staa huyo ambaye ni mchezaji wa kwanza raia wa Afrika Kusini kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara na ndiye aliyepokelewa kwa shangwe kubwa na mashabiki wa Yanga katika utambulisho wa wachezaji wote wa timu hiyo kwenye tamasha la klabu hiyo lililofanyika wikiendi iliyopita amekuwa akipewa matumaini makubwa sana na mashabiki.

Kwenye tamasha la timu hiyo maarufu kama Wiki ya Mwananchi, Skudu licha ya kucheza kwa dakika 45 kwenye mchezo dhidi ya Kaizer Chiefs lakini alifanikiwa kuwashawishi mashabiki wa timu yake akitumia ufundi wa kuuchezea mpira kwa ustadi wa hali ya juu.

Skudu amekiambia chanzo kuwa licha ya mashabiki kumpokea kwa shangwe lakini bado ana kazi kubwa ya kujituma ili kupata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kocha Miguel Gamondi huku pia akisubiri kuona ubora wa Simba.

Alisema Yanga ni timu kubwa na ina wachezaji bora hivyo pamoja na umaarufu alionao na upendo waliouonyesha mashabiki lakini kazi kubwa ni kupata namba uwanjani.

“Kwangu nasubiri sana kuwaona wapinzani kama Simba na Azam ili nijue wana ubora kiasi gani, lakini kwa ujumla lazima nikuhakikishie kuwa tuna timu bora.

“Ni kazi kubwa kupata namba hapa kwani wachezaji wengi wako vizuri na wote wanahitaji nafasi ya kucheza hivyo mtihani mkubwa ni kuonyesha uwezo utakaonifanya kucheza kwenye kila mchezo,” alisema staa huyo aliyejiunga na Yanga akitokea Marumo Gallats ya Sauzi na kuongeza:

“Naheshimu ubora wa wengine kwani najua tumekuja kwa ajili ya kuipa timu mafanikio na kitakachotupa nguvu ni ushirikiano na juhudi binafsi, lakini nafahamu kuwa natakiwa kuonyesha juhudi za hali ya juu kama nataka kucheza,” alisema Skudu.

SOMA NA HII  HII HAPA WIKIENDI NYINGINE YA KUBEBA MTONYO KUTOKA MERIDIANBET....ZINGATIA ODDS HIZI TU...