Home Habari za Yanga Leo NYIE MNAIDHARAU YANGA KWAKUWA IPO KARIAKOO TU

NYIE MNAIDHARAU YANGA KWAKUWA IPO KARIAKOO TU

habari za yanga-NABI

MCHAMBUZI na Mwanachama wa Yanga Dominic Salamba amewamwagia maua yao Wananchi kwa kuwa na timu bora Afrika.

Salamba ameipatia sifa Yanga kutokana na kufanya makubwa sana, katika Ligi kuu kwa misimu mingi na michuano ya kimataifa kwa miaka ya hivi karibuni.

“Pata picha hii Yanga sc ingekuwa inapatikana Kenya, Congo, Rwanda, Burundi, Sudan au Uganda hivi tungeendelea kuichukulia poa?”

“Ni ubora gani tunautaka ili tuwape heshima yao na kuwa sehemu ya kujivunia kama Taifa?

Timu ina mifumo mizuri,viongozi imara, dira yao inaelezeka na kuonekana ikifuatiliwa.”

“Ni wakati wa kuwapa heshima yao,ndio mtetezi wa ukanda wetu huu hatuna timu bora kama wao kwasasa.”

“Nimeamua kusimama na ukweli na sio sifa za kijinga..”Amesema Dominic Salamba.

SOMA NA HII  MAJALIWA AING'ATA SIKIO TAIFA STARS AFCON 2017