Home Habari za michezo SIO SIMBA WALA YANGA ANAWEZA KUCHUKUA UBINGWA WA CAFCL.

SIO SIMBA WALA YANGA ANAWEZA KUCHUKUA UBINGWA WA CAFCL.

Wachambuzi wa michezo wameendelea kutoa maoni yao kuhusu timu za ndani zinashiriki michuano ya Kimataifa haswa kwa Simba na Yanga.

Moja kati ya wachambuzi hao ni Geofrey Lea ambaye ametoa kauli ya kwamba sio Simba wala Yanga anaweza kuchukua ubingwa wa CAFCL.

“Mo anasema ndoto yake kubwa ni Simba kuchukua ubingwa wa Afrika, je inawezekana?” Aliukiza Paul Mkai kwenye kipindi hii leo.

“Kinadharia Simba wanaweza kuchukua ubingwa wa Afrika, ila kiuhalisia bado hakuna klabu ya Tanzania inayoweza kuchukua ubingwa wa Afrika.

“Paul Mkai unanijua kwa muda mrefu, sinaga kawaida ya majibu mafupi, natamani kukwambia inaweza hata kupita miaka 50 kwa klabu ya Tanzania kuchukua ubingwa wa Afrika” Geof Lea

SOMA NA HII  AHMEDA ALLY:- VIONGOZI SIMBA TUNAPASWA KUJITAHMINI KWA HALI YA TIMU ILIVYO...