Home Ligi Kuu WAWILI WAMPASUA KICHWA KOCHA MKUU MTIBWA SUGAR

WAWILI WAMPASUA KICHWA KOCHA MKUU MTIBWA SUGAR


 BEKI wa kulia, Hassan Kessy kwa sasa anampasua kichwa Kocha Mkuu wa Klabu ya Mtibwa Sugar kutokana na kusumbuliwa na majeraha.

Mbali na Kessy pia mshambuliaji wake Salum Kihimbwa naye ni majeruhi na hawa wote walikwama kushiriki Kombe la Mapinduzi Visiwani Zanzibar kutokana na kutibu majeraha yao.

Hitimana Thiery ambaye ni kocha wa Mtibwa Sugar baada ya kupokea mikoba ya Zuber Katwila ambaye yupo zake ndani ya Ihefu FC kwa sasa ameliambia Spoti Xtra wameanza mazoezi bila ya uwepo wa nyota hao.

“Tumeanza mazoezi tayari kwa ajili ya mzunguko wa pili na imani yetu ni kwamba tutafanya vizuri ila sijaanza mazoezi na Kessy pamoja na Kihimbwa hapa tunasubiri waweze kurejea kwenye ubora wao ili waanze mazoezi na timu hivyo kwa sasa ninafikiria wale ambao watachukua nafasi zao,” alisema.

Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 11 ikiwa na pointi 22 baada ya kucheza jumla ya mechi 18 msimu wa 2020/21.

SOMA NA HII  RATIBA YA VIPORO LIGI KUU BARA IPO NAMNA HII