Home Habari za michezo SIMBA NA YANGA KUITEKA ALGERIA KWA WAKATI MMOJA

SIMBA NA YANGA KUITEKA ALGERIA KWA WAKATI MMOJA

Kwa mara ya kwanza, timu za Simba na Yanga zitakuwa nchini Algeria kwa wakati mmoja (ndani ya wiki moja) kwenye mechi za michuano ya CAF, kila timu ikiwa na kibarua chake.

Wiki hiyo ni ile yenye tarehe 6-8 mwezi Desemba mwaka huu, ambapo Simba itakwenda kucheza mchezo wa raundi ya pili hatua ya makundi Kombe la Shirikisho dhidi ya CS Costantine ambayo maskani yake ni katika mji wa Costantine….

Wakati Yanga ikiwa Algiers kucheza dhidi ya MC Alger, mchezo wa hatua hiyohiyo kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika…

Mechi hizi huenda zikapishana kwa siku moja hadi mbili lakini pia huenda zikapigwa katika miji tofauti ambayo ni

Costantine na Algiers.

Je, Simba na Yanga ‘kuivamia’ Algeria kwa wakati mmoja kusaka alama tatu za CAF, unapata picha gani????

Ratiba ya Simba iko hivi:-

28/11/2024: Simba vs Bravos

08/12/2024: Costantine vs Simba

15/12/2024: Simba vs Sfaxien

05/01/2025: Sfaxien vs Simba

12/01/2025: Bravos vs Simba

19/01/2025: Simba vs Costantine

Ratiba ya Wananchi Yanga;

26/11/2024: Yanga vs Al Hilal

06/ 12/2024: MC Alger vs Yanga

13/12/2024: Tp Mazembe vs Yanga

03/01/2025: Yanga vs Tp Mazembe

10/01/2025: Al Hilal vs Yanga

17/01/ 2025: Yanga vs MC Alger

SOMA NA HII  HUYU HAPA MTZ MWINGINE ATAKAYEINGIA KWENYE REKODI ZA LIGI YA MABINGWA ULAYA LEO...