Home Habari za michezo PAMOJA NA KUSHINDA GOLI TANO TANO….UNAAMBIWA GAMONDI HUKO YANGA HAJAONA KITU BADO….

PAMOJA NA KUSHINDA GOLI TANO TANO….UNAAMBIWA GAMONDI HUKO YANGA HAJAONA KITU BADO….

Habari za Yanga SC

KOCHA mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi ni kama ameanza kuwatisha wapinzani wake kutokana ubora wa kikosi chake mpaka sasa baada ya kusema kuwa bado kabisa hajaifikia ubora wa asilimia mia moja ya kikosi chake hivyo bado anakazi kubwa ya kuendelea kuijenga timu hiyo.

Gamondi ametoa kauli hiyo Yanga ikiwa imerejea katika maandalizi yake ya mchezo wa pili wa hatua ya kuwania kufuzu makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya El-Merreikh ya Sudan katika mchezo wa kwanza unaotarajia kupigwa Septemba 16,. mwaka huu nchini Rwanda

Gamondi alisema licha ya kuendelea kufanya vizuri katika michuano wanaoshiriki lakini bado hafikia asilimia mia moja kwa wachezaji wake kufanya anachokitaka ili kuweza kufikia malengo ya msimu huu.

Alisema bado hajafikiria asilimia anazohitaji kwa ubora wa kikosi chake, anaimani kwa muda mchache anaweza kupata matuamini na wachezaji kufanya kile anachowaelekeza.

“Tumebakiwa na wachezaji wachache kutokana na wengi kuwa katika majukumu ya timu za taifa kabla ya kurejea na kuendelea mikakati yetu, tumekuwa tukifanya mazoezi ufukweni kwa ajili ya kutaka kujenga stamina kwa wachezaji pamoja na kubadilisha mazingira kwa sababu maandalizi kujipanga kulingana na ubora wa wapinza wetu katika Ligi ya Mabingwa

Tumefanikiwa kuona ubora wao na wachezaji gani wakuwachunga, wanapokuwa nyumbani wanacheza vipi na hata ugenini. ” alisema Gamondi.

Aliongeza kuwa kwa wiki mbili alizokuwepo Tanzania ameona wachezaji wengi wenye vipaji ndani ya timu yake hilo ameliona na kuwapa nafasi ndani ya kikosi chake.

“Ni kweli Tanzania ina vipaji, hivi karibuni nilikuwepo Zanzibar nimeona wachezaji wenye kiwango kizuri, matarajio yangu msimu ujao nitakuwa sehemu y skauti ili kupata wachezaji wazuri na wazawa ambao watasaidia timu,” alisema kocha huyo.

Ofisa habari wa Yanga, Ally Kamwe alisema timu imeingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya mechi yao dhidi ya Al Merrikh kuhakikisha wanafanya vizuri kwa kupata matokeo mazuri ugenini kabla ya kurudiana nyumbani.

Alisema wachezaji wote ambao hawako kwenye majukumu ya timu ya Taifa wanaendelea na maandalizi ya mchezo wetu dhidi ya Al Merrikh kusaka ushindi katika mchezo huo ili kuja nyumbani kumaliza mchezo na kutinga makundi.

“Kocha Gamond anaendelea na mazoezi kujiandaa vizuri na kupeperusha bendera ya Taifa, hali ya Gift Freddy inaendelea vizuri ameondolewa kwenye majukumu ya timu ya taifa ya Uganda kwa sababu ya kupata majeraha madogo (Minor Injury) ambayo atakaa siku tatu nje ya uwanja.

Madaktari wa timu ya Uganda wametataarifu kuwa wamemruhusu Gift kurejea Tanzania na kocha wao ameshapata mbadala wake kuelekea mechi yao ya kufuzu AFCON dhidi ya Niger, “ alisema Kamwe.

Alisema nyota huyo kurejea Tanzania ndani ya hizi siku mbili na kuingia kwenye kikosi moja kwa moja kujiandaa na mechi yao dhidi ya Al Merrikh ambayo wanaenda kucheza Rwanda.

Kamwe alisema wanatarajia kucheza mechi moja ya kirafiki siku moja ya wikiendi kwa ajili ya kujiandaa kuelekea mechi yao dhidi ya Al Merrikh.

“Bado hatujajua tutacheza na timu gani lakini baada ya mechi hiyo, Septemba 14, mwaka huu kuelekea nchini Kigali, Rwanda na tayari kwa mchezo wetu huo kwenda kupeperusha bendera ya Tanzania katika mchezo wetu huo, alisema Kamwe.

SOMA NA HII  KISA TETESI ZA MNIGERIA WAO AKPAN KUJIUNGA NA SIMBA...COASTAL UNION WAIBUKA NA MADAI HAYA MAPYA...