Home Uncategorized KOCHA YANGA AMLILIA HERITIER MAKAMBO

KOCHA YANGA AMLILIA HERITIER MAKAMBO


KOCHA wa zamani wa timu ya Yanga, Azam FC na Singida United Hans Pluijm amesema kuwa itachukua muda mrefu kwa mbadala wa mshambuliaji wa Heritier Makambo kuvaa viatu vya mshambuliaji huyo ndani ya ligi.

Pluijm amesema kuwa kwenye suala la washambuliaji ambao wamezoea mazingira ya ligi ghafla ni pamoja na Makambo ambaye amekuwa ni injini ya mabao ndani ya Yanga hivyo itakuwa ngumu kwa atakayefuata kuvaa viatu vya Makambo.

“Mpira wa miguu una changamoto nyingi, sasa kwa mchezaji kama Makambo kuuzwa itachukua muda kwa atakayefuata kuaa viatu vyake kutokana na ukweli kwamba yeye alianza kuyazoea mazingira ya ligi.

“Busara ingetumika kumbakiza ndani ya Yanga ukizingatia kwamba imepata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa ilikuwa ni suala la kumuongezea maslahi bora ili aendelee kuitumikia Yanga,” amesema.

Makambo amejiunga na timu ya Horoya AC na kwa uoande wa washambuliaji ndani ya ligi ametupia jumla ya mabao 17.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA NYUMA GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA