Home Habari za michezo KIVULI CHA MAYELE KINAVYOMTESA GUEDE YANGA…MUSONDA AMESHINDWA….?

KIVULI CHA MAYELE KINAVYOMTESA GUEDE YANGA…MUSONDA AMESHINDWA….?

Habari za Yanga leo

Wakati jumba la ma onyeshe likiwa limebeba picha mbali mbali za Fiston Kalala Mayele, ni jina la Kennedy Musonda lilikuwa likiwekwa kando za frame za mfalme yule aliyetoweka na kutimkia kwa Mafarao wa Misri.

Ni kivuli cha Mkongomani Fiston Mayele kilitufanya tuamini miguu ya Kennedy Musonda isingeweza kuthubutu kuvaa viatu vya mfalme yule, bado tumeendelea kuamini hivyo mpaka leo.

Wakati mabaki ya kumbukumbu ya Fiston Mayele yakiendelea kutafuna mioyo ya mashabiki wa Yanga, Hafiz Konkoni aliibuka chambo kwenye kurejesha furaha. Wananchi walikopesha imani ambayo waliamini ingerudi na riba, lakini Konkoni hakuweza kulipa imani ile.

Joseph Guede anakuja wakati mioyo ya mashabiki wa Yanga imeshafubaa kwa mateso ya kukosa imani dhidi Mzize, Musonda na Konkoni. Mbaya zaidi Watanzania hatujawahi kusujudu neno ‘ngoja tumpe muda’. Si kwa Simba wala Yanga, mashabiki wanaweza kukuhukumu kwa dakika ishirini tu ulizocheza.

Kwa Joseph Guede kwake si wakati wa kusikiliza kivuli cha Filton Mayele. Ni ukweli usiofichika inabidi kwanza ajiweke fit kuanzia akili hadi mwili ili awe bora kuliko jana.

Wakati huu imani ya wananchi iliyozaliwa kwenye mifumo yao ya ufahamu inaweza kuwalipa na fidia. Uchezaji wake, nguvu, stamina, ataweza kumudu vyema ligi letu. Wananchi waamini kwenye muda.

SOMA NA HII  YANGA vs CLUB AFRICAIN:...FANYEENI YOOTEE LAKINI HILI LA MWAMUZI MKILISAHAU IMEKULA KWENU....