Home Uncategorized TAULO LA JUMA KASEJA LAZUA ‘TIMBWILI’ MBEYA

TAULO LA JUMA KASEJA LAZUA ‘TIMBWILI’ MBEYA

 


 KIPA namba moja wa Klabu ya KMC, mkongwe Juma Kaseja aliingia kwenye mzozo na shabiki mmoja anayedhaniwa kuwa ni wa Klabu ya Mbeya City. 

Shabiki huyo aliibuka ndani ya Uwanja wa Sokoine dakika za lala salama baada ya kuona lango la KMC timu yake inakwama kufunga bao kwa kukosa nafasi nyingi jambo lililomfanya ahitaji kusepa na taulo la Kaseja lililokuwa langoni.

Baada ya Kaseja kuona taulo linasepa aliamua kuacha lango wazi huku mpira unaendelea na kufuata taulo lake na kulibakiza taulo lake langoni.


Kuhusu ishu hiyo Kaseja amesema:”Taulo halikuwa langu jambo lililonifanya nilifuate kwa yule ambaye alichukuwa kwa kuwa sikuwa na chaguo.


“Nilifanya hivyo kutokana na hali ya hewa ya Mbeya niliazima hotelini ili niwe nafuta gloves zangu zikilowana au mvua ikizidi niwe najifuta usoni hakuna kingine kwani ningemuachia ningedaiwa hotelini.”


Kwenye mchezo huo timu zote zilitoshana nguvu bila kufungana na kugawana pointi mojamoja.

SOMA NA HII  POLISI TANZANIA YAZITAKA POINTI TATU ZA DODOMA FC, MMOJA KUUKOSA MCHEZO