Home Simba SC KILICHOMWONDOA BOCCO SIMBA HIKI HAPA

KILICHOMWONDOA BOCCO SIMBA HIKI HAPA

IMEBAINIKA kuwa kilichokuwa kikimsumbua nahodha wa klabu ya Simba, John Raphael Bocco si majeraha kama ilivyokuwa ikiripotiwa hapo awali bali ni magonjwa mengine ya kiafya.

Bocco anayekamatia nafasi ya pili kwenye chati ya wafungaji bora msimu huu akiwa na mabao nane, juzi Ijumaa alirejea kwa mara ya kwanza uwanjani kuichezea Simba kwenye mchezo wa kombe la FA dhidi ya African Lyon hii ni baada ya kukosekana tangu Januari 6, mwaka huu.

Akizungumzia hali ya nahodha huyo, Meneja wa kikosi cha Simba, Abbas Ally amesema, Bocco  sasa yuko fiti kwa ajili ya kuendelea kukisaidia kikosi chake kupata matokeo uwanjani.

“Nahodha wetu Bocco amerejea tayari kikosini baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu, na kukosekana kwake uwanjani kwa muda wote uliopita hakukuwa na uhusiano wowote na majeraha, bali ni changamoto nyingine za kiafya za kawaida,”

SOMA NA HII  AHMED ALLY:- MVUA NI ISHARA NZURI KWA SIMBA....