ga, Kelvin Yondani ambaye aliwahi kuwa nahodha wa kikosi hicho inaelezwa kuwa miongoni mwa mabeki anaowakubali ndani ya Bongo ni pamoja na beki chipukizi anayekipiga ndani ya Mtibwa Sugar Dickson Job.
Yondani anayevaa jezi namba tano mgongoni inaelezwa kuwa ameishauri Yanga kuinasa saini ya chipukizi huyo ili waungane ndani ya kikosi cha mabingwa wa kihistoria.
“Miongoni mwa mabeki anaowakubali Yondani ni pamoja na yule Job anayecheza Mtibwa Sugar, huenda akaitwa mezani ili kuzungumza na Yanga juu ya yeye kutua Jangwani,kwani tayari kuna watu wameanza mazungumzo naye” ilieleza taarifa hiyo.
Job amesema:” Sijazungumza na kiongozi yoyote wa timu ya Yanga kuhusu mkataba wangu ila kuna watu ambao sio viongozi wamekuwa wakinipigia simu kuuliza juu ya suala hill.”