Home Habari za michezo SIMBA YAINGIA MITINI…YANGA YAPATIWA USHINDI WA MEZANI…VURUGU WACHEZAJI NA POLISI

SIMBA YAINGIA MITINI…YANGA YAPATIWA USHINDI WA MEZANI…VURUGU WACHEZAJI NA POLISI

Habari za Michezo leo

Aprili 20, 2024, watani wa jadi wa soka la Tanzania, Yanga na Simba, watakutana katika muendelezo wa ligi kuu kwa msimu wa 2023/24.

Watani hawa wanakutana kwa mara ya kwanza tangu Yanga amtambie Simba kwa kipigo cha mbwa mwizi cha 5-1, Novemba 5, 2023.

Katika historia yao, wababe hawa wa soka la Bongo wameshakutana mara nyingi sana na kufungana mechi nyingi, lakini vipigo vikubwa kama cha Novemba 5, viko vichache.
Yanga 5-0 Simba (Sunderland) – 1968
Simba 6-0 Yanga – 1977
Simba 4-1 Yanga – 1994
Simba 5-0 Yanga – 2012
Yanga 5-1 Simba – 2024

Sasa kuanzia leo tutakuwa tukikuletea simulizi za mchezo ambao huwa unafuata baada ya mechi ya kipigo kikubwa, tangu wamba hawa waanze kukutana kwenye ligi ya Tanzania iliyoanza 1965.

BAADA YA YANGA 5-0 SIMBA – 1968 Huu ulikuwa mchezo uliopangwa kufanyika Machi 3, 1969. Mchezo
huu ilikuwa wa kwanza tangu Simba, wakati huo ikiitwa Sunderland, ifungwe 5-0 na Yanga, Juni Mosi 1968.

Matarajio ya wengi yalikuwa kuona Simba ikilipa kisasi cha aibu waliyoipata katika mchezo uliopita, lakini haikuwa hivyo….Simba wakaingia mitini na Yanga kupata ushindi wa mezani.
Ilikuwaje?

Hii ni moja ya mechi zinazotukumbusha namna mpira wetu ulikuwa na utaratibu wa hovyo miaka hiyo.
Mwaka 1969 ligi yetu, wakati huo ikiitwa

KLABU BINGWA YA TAIFA

ilikuwa na mikasa mingi sana.
Simba walicheza na African Sports ya Tanga na kutoka sare ya 1-1 katika moja ya mechi za mwanzoni mwa msimu.

Baadae ikabainika Sports ambao wakati huo walikuwa moja ya timu kubwa nchini, walimchezesha kipa wa timu ya Ujamaa ya huko huko Tanga ambayo pia ilikuwa ikishiriki ligi hiyo.

Simba wakakata rufaa FAT wakitaka wapewe ushindi kutokana na kosa hilo.
Hata hivyo, Sports hawakukurupuka kumchezesha kipa huyo kwani waliomba idhini ya FAT kufanya hivyo na walikubaliwa.

Sababu ya kuomba idhini ilikuwa changamoto zilizowakabili. Kipa wao namba moja alisafiri na timu ya taifa, na kipa namba mbili alikuwa na maradhi ya macho.

Lakini hata hivyo, FAT iliwakubalia kumtumia kipa mwingine bila kuuliza jina lake na alikotoka.

Baadaye FAT ikakiri kwamba ilikosea kuwaruhu Sports kumtumia kipa ambaye hawakumjua.

Kosa hilo pamoja na makosa mengine ya kiutawala (administrative errors) yakaifanya serikali iuvunje uongozi wote wa FAT na kuunda kamati ya muda kuendesha mpira.

Simba wakaibuka wakitaka wapewe ushindi kwenye ule mchezo wa Sports kwa sababu yule kipa hakustahili.

Kuonesha msisitizo wakasema hawatocheza mechi ya watani iliyopangwa kufanyika Machi 3, 1969, kama hawatopewa ushindi.

Kamati mpya ilipoanza kazi, ikairudishia Simba fedha walizolipa kukata rufaa.

Simba wakapata matumaini yawezekana watapewa ushindi wao.
Hata hivyo, kamati haikuona sababu ya kuwapa Simba ushindi ikisema hakuna ushahidi wa moja kwa moja unaothibitisha Simba waliathirika na kipa yule kucheza.

Simba wakafanya kama walivyoahidi kwamba hawatocheza dhidi ya Yanga, Machi 3, 1969… hawakutokea uwanjani.
Kama ya muda ya FAT ikaipa Yanga ushindi wa mezani na kuitoza Simba faini ya shilingi mia tano ambazo zilipaswa kulipwa haraka la sivyo timu hiyo isingeruhusiwa kuendelea kushiriki ligi.

Kufikia hapo hali ilionekana İnsekela kubaya. Ikabidi watu wazima wakae kikubwa na kuyazungumza.

Simba ikaondolewa faini na ikaruhusiwa kuendelea na ligi… lakini hawakupewa ule ushindi walioulilia sana, dhidi ya Sports.9

Kwa hiyo msimu wa kwanza baada ya kile kipigo, jamaa hawakukuta.

Wakatakiwa kukutana msimu mwingine tena, 1970, lakini nao ukapita kapa kwa sababu msimu huo ligi haikufanyika.
Kisa cha ligi kutofanyika ni mgogoro uliozaliwa kutokana na mabadiliko ya uendeshaji wa ligi yaliyoletwa na FAT.

Kwa miaka mingi, tangu kuanza kwake mwaka 1965, ligi ilitawaliwa zaidi na timu za mitaani.

Lakini mwaka 1970 FAT ikafungulia milango timu nyingi za taasisi kushiriki ligi.

Hapo ndipo timu kama Ngome (TPDF) ya jeshi la wananchi, Polisi, Magereza (Prisons), Cargo n.k zikapata nafasi ya kushiriki ligi.

Ujio wa timu hizi ukazifanya timu za mitaani kama Simba, Yanga na Cosmopolitan kukosa wachezaji kwani wachezaji wao walikuwa wakifanya kazi kwenye taasisi hizo hasa Cargo,

kampuni ya mizigo bandarini, na sasa walitakiwa kuchezea timu za kazini kwao.

Timu za mitaani zikagoma kushiriki ligi. Pia mfumo wa uchezaji ulikuwa mgumu sana.

FAT, kwa nia njema, ilitaka ligi ichezwe nchi nzima lakini hata hivyo hiyo isingewezekana kutokana na miundombinu.

Hati wakati wa kuwasilisha CAF Bingwa wa Tanzania kushiriki Klabu Bingwa Afrika msimu ujao ulipofika, ligi ilikuwa haijafika hata nusu…FAT ikaamua kuivunja na kutuma jina la Yanga CAF kwa kama wawakilishi wapya kwenye klabu Bingwa.

FAT walifanya hivyo kwa sababu Yanga walikuwa mabingwa wa 1969 hivyo waliwaacha waendelee kushiriki Afrika. Kwa hiyo msimu wa 1970 nao ukapita bila watani kukutana, kama ilivyokuwa kwa msimu wa 1969.

Hii ina maana tangu wakutane Juni Mosi, 1968, watani hawakukutana tena kwa misimu miwili mbele.
Msimu mwingine wa 1971 ukaja na matumaini ya watani kukutana tena yakaja.

Wakati huo ligi ilianzia ngazi ya mkoa, na zinazofuzu hapo zinaenda kushiriki ligi ya taifa…huko ndiko bingwa alikuwaanapatikana.

Yanga na Simba wakakutana kwenye kuwania ubingwa mkoa wa Pwani, na Yanga kushinda 2-0. Wakati huo Dar es Salaam ilikuwa ndani ya Mkoa wa Pwani.

Hili likawa pambano la kwanza la watani tangu 1968, hata hivyo halikuwa katika hadhi kama yake mengine ambayo yalikuwa katika kuwania ubingwa wa taifa.

Na bahati mbaya ni kwamba hawakukutana tena kwenye ligi ya taifa kutokana na matatizo yale yale ya kiutawala.

Baada ya kukamilika kwa ligi ya mikoa, ligi ya taifa ikaanza na timu zikacheza michezo kadhaa. FAT wakaibuka katikati na kusema wanabadili mfumo. Timu za Dar es Salaam zicheze zenyewe kwanza.

Timu hizo zilikuwa Simba, Yanga, Cosmopolitan na Tambaza. Hizi ndiyo zilikuwa timu zenye nguvu zaidi Dar Es Salaam wakati ule. Simba wakagomea agizo hili wakisema limekuja kuvuruga ligi ambayo ilikuwa inaendelea vizuri…ikajitoa kwenye ligi.

Hii ndiyo sababu ya watani kutokutana tena kitaifa, tangu 1968. Mechi ya ligi ya taifa ilikuja kufanyika Juni 18, 1974, nusu fainali ya ligi ya taifa.

Hata hivyo mechi hii ilivunjika kipindi cha pili wakati Yanga wakiongoza 1-0 kwa bao la Leonard Chitete. Sababu za kuvunjika ni vurugu zilizifanywa na mchezaji wa Simba, Emmanuel Mbele “Dubwi”, aliyemrukia vibaya Gibson Sembuli wa Yanga.

Mbele pia aliwahi kusababisha mechi kuvunjika mwaka 1968, na kusababisha kurudiwa Juni Mosi na Yanga kushinda 5-0. Baada ya Mbele kumfanyia shambulio la kudhuru mwili Sembuli, vurugu zinaibuka uwanjani kati ya wachezaji kwa wachezaji na polisi kuvamia uwanja na kuvunja mechi.

Yanga wakapewa ushindi wa mezani kwa sababu Simba ndiyo walisababisha vurugu. Pambano la kwanza la kitaifa lililomalizika lilifanyika Juni 23, 1973, mchezo wa nusu fainali ya ligi ya taifa.

Mchezo huu ulifanyika uwanja wa taifa (sasa uhuru) na Simba kushinda 1-0, bao la nahodha Haidar Abeid dakika ya 68.

Kwa maana rahisi ni kwamba tangu Juni Mosi 1968, watani wa jadi hawakukutana katika ligi rasmi hadi Juni 23, 1973….miaka mitaano baadaye!

SOMA NA HII  UCHAGUZI WAITIKISA SIMBA SC...WANACHAMA WAMCHAGUA MWENYEKITI....MATABAKA YAZALIWA