Uongozi wa klabu ya Yanga, umesema fedha zinazotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan zimeongeza moli kubwa kwa wachezaji kuipigania timu yao.
Hayo yamesemwa na Mratibu wa Yanga, Hafidh Salehe, wakati wa uchezeshaji wa droo ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam hatua ya robo fainali, iliyofanyika juzi katika ofisi za Azam Media.
Salehe alisema kipindi cha nyuma timu yao ilikuwa inaishia hatua ya awali ya michuano ya Kimataifa, lakini sasa vijana wamekuwa na hamasa kubwa ya kuipigania nembo ya timu yao.
“Sisi kwa sasa tunashukuru kwa hamasa hii, unawaona kabisa wachezaji wanavyopambana ili kuipatia timu matokeo mazuri uwanjani, hivyo tunashukuru kwa kila kitu kinachochangia ushindi wetu.