Home epl CAVAN KUPEWA MKATABA MNONO UNITED

CAVAN KUPEWA MKATABA MNONO UNITED


 KLABU ya Manchester United inajiandaa kumpa mkataba ambao utakuwa na mshahara mnono mshambuliaji wao Edinson Cavani.

Awali ilikuwa inaelezwa kuwa Cavani alikuwa anajiandaa kuondoka ndani ya kikosi hicho mwishoni mwa msimu.

Kutokana na kiwango cha nyota huyo kuzidi kuimarika kimewafanya United wafikirie kumpa kandarasi mpya nyota huyo.

Taarifa kutoka ndani ya United kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail la Uingereza limeeleza kuwa mabosi wa United wanahitaji kumpa dili la pauni milioni 250,000 sawa na shilingi milioni 810.

Alijiunga na United akitokea kikosi cha PSG ya Ufaransa msimu huu. Jana wakati timu yake ikishinda mabao 3-1 dhidi ya Aston Villa alitupia pia bao moja.

SOMA NA HII  KUMBE SOLSKAJER HAFURAHISHWI NA KAMPENI ZA NEVILE