Home Uncategorized MAGUIRE:TUMEUMIA KUFUNGWA LIGI YA MABINGWA ULAYA

MAGUIRE:TUMEUMIA KUFUNGWA LIGI YA MABINGWA ULAYA

 


NAHODHA wa Klabu ya Manchester United Harry Maguire amesema kuwa hawakustahili kufungwa usiku wa kuamkia leo mabao 3-2 dhidi ya RB Leipzig kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya. 

United ilianza kuokota nyavuni bao mapema dakika ya 2 kupitia kwa Angelino na lile la pili lilifungwa dakika ya 13 na Amadou Haidara na kuwafanya waende mapumziko wakiwa nyuma kwa mabao 2-0.


Kipindi cha pili United iliokota nyavuni bao la tatu kupitia kwa Justin Kluivert dakika ya 69 na United walipata penalti dakika ya 80 iliyofungwa na Bruno Fernandes na lile la pili walipewa zawadi baada ya Ibrahima Konate kujifunga dakika ya 82.


Kichapo hicho Uwanja wa Red Bull Arena kinawafanya United chini ya Kocha Mkuu, Ole Gunnar kufungashiwa virago kwa kuwa walikuwa wanahitaji sare ili wajihakikishie nafasi ya kufuzu 16 bora ndani ya kundi H ila mambo yalikuwa magumu kwao.


Maguire amesema:”Tumeumia kutolewa na hatukupaswa kufungwa lakini kwa kuwa ni matokeo hatuna chaguo,”.

SOMA NA HII  CLUB 361 INAKULETEA MAPAMBANO YA UBINGWA AFRIKA MASHARIKI NA KATI