Home Uncategorized SIMBA KUFUNGIWA MIAKA MITATU KUFANYA USAJILI NA FIFA

SIMBA KUFUNGIWA MIAKA MITATU KUFANYA USAJILI NA FIFA


 UONGOZI wa Namungo umesema kuwa kwa mujibu wa barua ambayo wametumiwa na FIFA kuhusu mchezaji wao Shiza Kichuya kuna uwezekano wa Klabu ya Simba kufungiwa kufanya usajili kwa muda wa miaka mitatu ikiwa hawatatimiza vigezo vilivyopo kwenye barua hiyo.


Kichuya ambaye kwa sasa anacheza ndani ya Namungo FC ambayo leo ina mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United alisajiliwa akiwa ni mchezaji huru baada ya Simba kumuweka kando mkataba wake wa miezi sita ulipokwishwa.


Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Namungo FC, Kindamba Namlia amesema kuwa usiku wa kumakia leo wamepokea barua kwa njia ya email ambayo imeeleza kuwa mchezaji huyo hataruhusiwa kutumika ndani ya Klabu ya Namungo kwa kuwa alisajiliwa akiwa na matatizo ya kimkataba na timu yake ya zamani ya Pharco ya Misri.


Kidamba ameongeza kuwa Simba imeambiwa ilipe faini kwa kosa la kumsajili mchezaji wakati akiwa na mkataba huku wao Namungo wakizuiwa kumtumia mchezaji huyo mpaka fedha hizo zitakapolipwa.


Habari zimeeleza kuwa kiasi ambacho Simba inatakiwa kulipa ni milioni 300 kwa kosa la kumsajili mchezaji ambaye mkataba wake haujaisha na bila kuwasiliana na timu ambayo ilikuwa inammiliki mchezaji.


Kichuya kwa msimu wa 2019/20 alipotua ndani ya Simba bado hakuwa na nafasi kikosi cha kwanza chini ya Sven Vandenbroeck na walisajiliwa kwa wakati mmoja na Luis Miquissone zama za Mtendaji Mkuu, Senzo Mbatha ambaye kwa sasa yupo Yanga.


Luis bado anaendelea maisha yake ndani ya Simba huku Kichuya akiendelea na maisha yake ndani ya Namungo ambayo inashiriki Kombe la Shirikisho.

Namlia amesema:”Sisi tulimsajili akiwa mchezaji huru hivyo bado kuna vitu ambavyo havipo sawa kwa kuwa ni wenye mamlaka wamesema basi tuna kazi ya kufuatilia na kukaa chini kujua kwa sababu haya ni masuala ya sheria.

“Hatukukurupuka kufanya usajili hivyo inabidi ujiulize kwa nini tulipata kibali cha kumtumia, kwa kuwa ni mamlaka basi tutafuata utaratibu ila tutaumia kumkosa Kichuya kwa sababu tayari alishaingia kwenye mfumo,” .

SOMA NA HII  MAMBO YAZIDI KUWA MOTO, KABWILI AHITAJIKA KAMATI MAALUM