Home Yanga SC HAYA HAPA MAJUKUMU MAPYA YA CARLINHOS YANGA

HAYA HAPA MAJUKUMU MAPYA YA CARLINHOS YANGA

 


KOCHA mkuu wa klabu ya Yanga, Cedric Kaze ameamua kumbadilishia majukumu kiungo mshambuliaji wa klabu hiyo raia wa Angola, Carlos Carlinhos kwa kumtoa katikati na kumtaka acheze kwa kutokea pembeni.

Licha ya kutumika kama namba kumi kwa muda mrefu tangu atue ndani ya kikosi cha Yanga, lakini katika mchezo uliopita wa kujipima nguvu dhidi ya African Sports uliopigwa katika uwanja wa Azam Complex Chamazi, jijini Dar es Salaam Carlinhos alionekana akicheza kutokea pembeni.

Kuhusiana na maamuzi hayo kocha Kaze amesema kupitia mbinu zake anadhani Carlinhos atakuwa bora zaidi akicheza katika eneo la pembeni, kulinganisha na katikati.

“Carlinhos katika mbinu zangu amekuwa akionyesha kiwango kizuri zaidi anapocheza akitokea pembeni kulinganisha na anapotokea eneo la katikati ya uwanja, na baada  ya kurejea nimepanga kumtumia zaidi katika eneo hilo kwa kuwa nadhani atafanya makubwa,”

SOMA NA HII  YANGA KUFANYIWA SAPRAIZI HII...HAIJAWAHI TOKEA BONGO...MABOSI WAPAGAWA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here