Home Habari za michezo UNAAMBIWA HUKO JANGWANI NI MWENDO WA SUPU TU ……. HERSI ATOA CHAPATI...

UNAAMBIWA HUKO JANGWANI NI MWENDO WA SUPU TU ……. HERSI ATOA CHAPATI 5000

Mashabiki na wanachama wa Klabu ya Yanga wamejitokeza kwa wingi kunywa supu leo Jumapili Novemba 12 2023 katika ofisi za makao makuu ya klabu hiyo zilizopo Jangwani, Dar es Salaam kama walivyokuwa wametangaziwa.

Hafla hii inakuja baada ya kumkanda mtani wao Simba SC kwa bao 5-1 katika mechi ya Ligi Kuu ya NBC Jumapili iliyopita katika Dimba la Mkapa na kuzawadiwa ng”ombe 10 ambao wameamua kuwachinja na kunywa supu.

Aidha Rais wa Yanga Eng. Hersi Said amewanunulia chapati 5000 mashabiki wote waliojitokeza kunywa supu leo Jangwani.

SOMA NA HII  SIMBA WAANZA KUSHUSHA VIFAA....ONANA APEWA MIWILI ....BRUNO GOMES WA SINGIDA AITWA DAR CHAP...