Home news KISA SIMBA….YANGA WAJA NA MPANGO WA KUWACHUNGUZA WACHEZAJI WAKE WASIHUJUMU TIMU

KISA SIMBA….YANGA WAJA NA MPANGO WA KUWACHUNGUZA WACHEZAJI WAKE WASIHUJUMU TIMU


YANGA imeshtuka kusikia watani wao Simba nao wametupwa nje ya Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini wakafichua mpango maalum wa kuwabana mastaa wao katika kuleta ufanisi zaidi katika msimu huu.

Yanga imeshushwa kutoka kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara na Polisi Tanzania, lakini wakilingana kila kitu ila wakitiofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa na sasa inajiandaa kuvaana na Azam FC.

Polisi iliifumua Ruvu Shootingi nyumbani kwao, Uwanja wa Mabatini, Pwani kwa bao la Vitalis Mayanga dakika ya 78 na mabosi wa Yanga wakaona wapange jeshi lao vizuri.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Yanga, Dominic Albinus ameliambia Gazeti la  Mwanaspoti, ingawa timu yao imeanza vyema ligi, lakini kuna mpango mgumu wa kuwabana nyota wao akiwamo kina Fiston Mayele, Djuma Shaban na wengine wote kwa kila kitu wanachokifanya ndani ya msimu huu.

Albinus alisema zoezi la kukusanya takwimu za ubora wa kila dakika ya mchezaji anayocheza uwanjani, pia hata wale ambao watakosa kucheza nao watakuwa wanaitwa kujitetea katika vikao vya ufundi.

“Tunashukuru kwa timu yetu kuanza vyema ligi lakini nikuambie hilo haliji kwa urahisi kuna uwajibikaji mkubwa unaotakiwa kufanyika kwa wachezaji wetu wote,” alisema Albinus.

“Kila mchezaji kuna takwimu zinazochukuliwa katika kila mchezo tunaocheza, zipo zinazochukuliwa na benchi la ufundi, pia zipo tunazozichukua wenyewe na baada ya hapo tunazijadili kwa pamoja tukizilinganisha kwa usahihi wake.

Albinus ambaye kitaaluma ni kocha alisema ripoti hizo zinakutanishwa kila baada ya robo za mechi zao za nusu ya msimu na kama kutakuwa na wachezaji watakaoonekana kuyumba ataitwa na kuulizwa matatizo yake kisha kamati ya ufundi inayapima.

“Hizi takwimu tutakuwa tunazitumia kuzijadili kila robo ya nusu msimu na tukikutana tunawahoji makocha kwa nini huyu mchezaji flani yuko chini na sababu tutakazozipata pia tutamwita mchezaji husika naye ajieleze.

“Lengo hapa ni kutaka kuona kila mchezaji anakuwa na uwajibikaji na kama tutaona shida inazidi basi tutaangalia kuachana naye inaweza kuwa katikati ya msimu au hata mwisho itategemea na ubora ambao tutaugundua kwake.

SOMA NA HII  BAADA YA KUANDAMWA SANA....MWAMUZI WA YANGA SAUZI AOMBA RADHI...AFUNGUKA A-Z KILICHOTOKEA...

Kigogo huyo aliongeza, mpango huo ndio unaowafanya sasa wachezaji wao kila mchezo kuonekana wako moto kwa kupambana katika mechi zao za ligi huku pia makocha nao wakiwa na kipimo chao.

“Hili hatufanyi tu kwa wachezaji hata makocha nao wanakuwa na ripoti zao na watu wanaona Yanga inashinda lakini wajue kwamba wachezaji wanaopata nafasi wanalitambua hili,kila mmoja sasa anajituma katika timu kuhakikisha anajiweka katika mazingira salama.”