Home Ligi Kuu WIKI KADHAA TOKA WAWE WADHAMINI….NEMBO YA NBC YAZUA UTATA KWA TIMU ZA...

WIKI KADHAA TOKA WAWE WADHAMINI….NEMBO YA NBC YAZUA UTATA KWA TIMU ZA LIGI KUU..


WAKATI Bodi ya Ligi (TPLB) ikizipiga mkwara mzito klabu za Ligi Kuu Bara kwamba kama hazitavaa nembo ya mdhamini Mkuu (NBC) basi zitapigwa faini ya Sh 1milioni, baadhi ya klabu zimedai hazijui watazipata wapi nembo hizo kwani hawajui zilipo.

Mtendaji Mkuu wa TPLB, Almasi Kasongo Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania, (TPLB) alisema wametoa taarifa kwa klabu zote za ligi na kanuni inayoeleza kuwa kama hawatafanya hivyo watatozwa faini.

“Kutokana na ucheleweshwaji wa makubaliano ya mkataba mpya na wadhamini wetu tulishindwa kuanza mapema kwa timu kuwapa kipaumbele kwa kuweka nembo hiyo kwenye bega, lakini mara baada ya kukamilika tulitoa taarifa kwa klabu kuwa ikifika raundi ya nne wanatakiwa kukamilisha hilo,” alisema Kasongo na kuongeza;

“Kanuni ndio italifanyia kazi suala la adhabu kulingana na ilivyopitishwa na kwa kuwa taarifa kwa klabu zilitolewa mapema atakayekiuka hatakuwa na namna ya kujitetea kanuni itafanya kazi maana ya kamati kukaa na kuamua nini cha kufanya,” alisema.

Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Geita Gold FC, Revinus Ntare aliliambia Mwanaspoti, hawajapata taarifa zozote kuhusiana na suala la nembo hadi sasa na hazijawafikia.

“Hii taarifa ya kutozwa faini kama hatutaweka nembo ya mdhamini begani ndio kwanza nazipata kwako, kwani hata hiyo nembo yenyewe hatuna,” alisema Ntare wakati Katibu wa Kagera Sugar, Masoud Ally aliungana na kauli ya Ntare kuwa na wao hawajapata na hawafahamu watazipata wapi hivyo kuhusiana na adhabu ya Sh1 milioni endapo hawatakuwa na nembo hiyo watakuwa wameshtukizwa kwani nayo pia hawana.

“Tupo mwishoni mwa nchi kabisa huku hatuelewi kinachoendelea hiki unachoniambia kuhusiana na adhabu kwa mujibu wa kanuni endapo hatutakuwa na nembo raundi ya nne nakusikia wewe, sina taarifa nacho na hata hiyo nembo yenyewe sijui inapatikana wapi,” alisema.

Wakati viongozi hao wakifunguka hayo wenzao wamekuwa kinyume nao kwani wamefunguka kupata taarifa za nembo Oktoba 16 na kupewa kanuni ya kutozwa faini hiyo kama hawatakamilisha.

SOMA NA HII  HEE...GSM KACHOMOA BETRI HUKO..KISA UBINGWA..MASTAA YANGA WASHTUKIWA...NABI AWATAJA WOTE..

Katibu wa Dodoma Jiji, Johnson Fortunatus alisema wamefanyia kazi maagizo waliyopewa na bodi na wanatarajia kuonekana na nembo ya mdhamini kwenye michezo inayofuata ili kukwepa adhabu kwa mujibu wa kanuni na kuwapa kipaumbele wadhamini.