Home Habari za Simba MASTAA HAWA 9 WATEMWA SIMBA…MASHINE HII HATARI KUTUA MSIMBAZI

MASTAA HAWA 9 WATEMWA SIMBA…MASHINE HII HATARI KUTUA MSIMBAZI

Habari za Simba leo

Klabu ya Simba Sc itaachana na nyota tisa mwishoni mwa msimu huu akiwemo kipa mmoja, mabeki wawili, viungo wawili, mawinga wawili na washambuliaji wawili.
Imeelezwa kuwa wachezaji watakaotemwa baadhi ni wachezaji wa zamani na baadhi ya waliosajiliwa hivi

karibuni kwa ajili ya kupisha wengine kusajili kuboresha timu hiyo kwa msimu ujao wa mashindano.

Taarifa za uhakika zilizotufikia kuwa viongozi wa klabu tayari wanatafuta wachezaji wa ubora wa juu ambao watasajiliwa na tayari majina matatu ambayo yamethibitishwa yapo kwenye meza ya kwa ajili ya kujadiliwa.

Chanzo hicho kimesema kuhusu kocha mpya anayekuja kuchukuwa nafasi ya Abdelhak Benchikha, upo katika mchakato huku baadhi ya majina yanajadiliwa.

“Moja ya jina limejadiliwa hivi karibuni ni Florent Ibenge wa Al Hilal ya Sudan, licha ya kuwepo kwa majina mengine, suala la Kibu (Dennis) uongozi unafahamu ushawishi kutoka kwa klabu fulani ambao wanataka kumsajili.

Kwa sasa ofa rasmi ya klabu inawasilishwa kuna mkutano na nyota huyo pamoja na viongozi umepangwa wiki ijayo kuongelea mustakbali wake lakini ni kuangalia na wachezaji wengine ambao mikataba yao imefikia tamati na kuongezwa,” amesema chanzo hicho.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema wanachokifany sasa ni kubaki na wale bora wenye moyo
wa kuitumikia klabu hiyo.

SOMA NA HII  ALHAMISI YA KIJANJA NA MKWANJA WA MERIDIANBET UKO KWENYE ODDS HIZI HAPA...