Home Yanga SC SAIDO NJE MWEZI MZIMA YANGA

SAIDO NJE MWEZI MZIMA YANGA

 

NYOTA mpya kunako kikosi cha Yanga, Saidi Ntibanzokiza ‘Saido’ raia wa Burundi, imebainika kwamba atakaa nje ya dimba kwa takribani mwezi mmoja akiuguza majeraha aliyoyapata katika michuano ya Kombe la Mapinduzi iliyomalizika Januari 13, mwaka huu.

Katika michuano hiyo ambayo Yanga ilikuwa mabingwa, Saido alikuwa sehemu ya mafanikio hayo ambapo mechi ya fainali dhidi ya Simba, alipiga penalti ya mwisho na kuipa kombe la kwanza.

Akizungumza na Spoti Xtra, Ofisa Mhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz, alisema: “Kimsingi watu wanatakiwa watambue kwamba mchezaji siku zote anatumia miguu kuhakikisha anacheza, hivyo akipata maumivu anakuwa anahitaji muda mrefu wa kujitibu hasa kwa majeraha ya aina kama hii ya Saido ambaye anasumbuliwa na uvimbe kwenye maungio ya paja na kiuno ambapo mara nyingi hutibiwa kwa kutumia mionzi.

 “Mwenyewe anasema kwa sasa anajisikia vema, ilitakiwa kwa majeraha yake akae miezi miwili, lakini anatarajia kurejea uwanjani ndani ya mwezi mmoja.”

SOMA NA HII  YANGA WASIMAMISHA MAZOEZI KWA SABABU YA MAGUFULI