Home epl HATMA YA POGBA NDANI YA UNITED YASHIKILIWA NA EUROPA

HATMA YA POGBA NDANI YA UNITED YASHIKILIWA NA EUROPA


 HATMA ya kiungo wa Manchester United, Paul Pogba inatarajiwa kujulikana mara baada ya fainali ya Europa League ambayo itapigwa Poland.

United inatarajiwa kucheza mchezo wa fainali ya Europa League, kesho, Mei 26 dhidi ya Villareal.

Kaka wa Pogba, Mathias amesema atazungumza na Kocha Mkuu wa United, Ole Gunnar Solkjaer baada ya fainali hiyo kuhusu nyota huyo raia wa Ufaransa.

Mkataba wa kiungo huyo ndani ya United unatarajiwa kumeguka mwaka 2022 Juni na wakala wake Mino Raiola alinukuliwa akisema kuwa staa huyo hana furaha ndani ya England.

Kaka wa Pogba amesema:”Kama Pogba atashinda taji la Europa League hapo ndipo tutazungumza hatma yake japo anahusishwa kwenda Barcelona pia,”.

SOMA NA HII  KOCHA ARSENAL AWASIFU WACHEZAJI WAKE