Home Uncategorized YAKUB NA ABAROLA MAMBO BADO MAZITO GHANA

YAKUB NA ABAROLA MAMBO BADO MAZITO GHANA


YAKUB Mohamed, beki kisiki pamoja na Razack Abarola, mlinda mlango namba moja wote wanaokipiga ndani ya Klabu ya Azam FC wamekwama kutua Bongo kutokana na zuio la Serikali ya nchini kwao Ghana.

Nyota hao waliibukia Ghana baada ya Serikali ya Tanzania, kusimamisha masuala ya michezo Machi 17 kutokana na janga la Virusi vya Corona ambalo linaivurugavuruga dunia.

Kwa sasa tayari Serikali ya Tanzania imeruhusu masuala ya michezo kuendelea baada ya kusema kuwa hali ya maambukizi imepungua.

Ofisa Habari wa Azam FC, Zaka Zakazi amesema kuwa ugumu wa kuwapata nyota hao unatokana na zuio la Serikali ya Ghana kuendelea mpaka sasa.

“Inakuwa ngumu kuwapata wachezaji wetu waliopo Ghana kwa kuwa kule bado kuna zuio la kutokutoka nje,’Locdown’ mpaka sasa hivyo tunasubiri kuona mambo yatakuaje ili waweze kuungana na timu,” amesema. 

Tayari Azam FC imeanza mazoezi kujiaanda na mechi zake za ligi ambapo kete ya kwanza itakuwa Juni 14 kwenye ligi dhidi ya Mbao FC, Uwanja wa Azam Complex.

SOMA NA HII  ZAHERA HUYU HAPA AMETUA NAMUNGO