Home Uncategorized YANGA YA GSM NI MOTO WA KUOTEA MBALI.. VIFAA VIPYA KUTOKA CONGO...

YANGA YA GSM NI MOTO WA KUOTEA MBALI.. VIFAA VIPYA KUTOKA CONGO NA KENYA VYANUKIA JANGWANI

KOCHA wa Yanga, Luc Aymael, amewaambia viongozi kwamba katika vitu ambavyo anataka msimu ujao ni kuona timu hiyo ikicheza mpira wa kasi na pasi nyingi.

Katika ripoti yake hata kwenye mikutano kwa njia ya video ambazo wamekuwa wakifanya kila mara, amewasisitiza kwamba anataka kuisuka Yanga tofauti kabisa na iliyozoeleka machoni mwa mashabiki na anataka vikombe.

Katika moja ya mapendekezo yake ni kuwa na winga matata anayejua kuzalisha krosi za mabao ambaye hata ikiwezekana ndani ya dakika 20 mpaka 40 mechi iwe wameisha.

Habari za uhakika ambazo Mwanaspoti imejiridhisha nazo ni kwamba kocha huyo amewapa Yanga majina mawili kwenye nafasi ya winga na kutokana na ubora wao na gharama mbalimbali watasajili mmoja tu kati ya hao.

Mmoja ni Mkongomani anayeichezea AS Vita, Tuisila Kisinda ambaye ndiye chaguo la kwanza la Eymael huku mwingine akiwa Mkenya, Harrison Mwendwa wa Kariobang Sharks ya Kenya.

Mwaka jana meneja wa Tuisila alifanya mazungumzo na Simba baada ya kocha aliyetimuliwa, Patrick Aussems kumpendekeza asajiliwe ili kusaidiana na Meddie Kagere.

Aussems aliwaambia Simba kwamba Mkongo huyo ni mzoefu na angeweza kuisaidia timu hiyo kimataifa na hata Senzo Mazingisa ambaye ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba alithibitisha kuwepo kwa dili hilo, lakini likafia juu kwa juu kutokana na masharti mazito ikiwamo mkwanja mrefu kuhitajika ili kunasa saini ya mdunguaji huyo.

Habari kutoka ndani ya kamati ya usajili wa Yanga zinasema kwamba, Eymael amewaambia vigogo wa GSM wapambane na meneja wa Tuisila hadi kuhakikisha kwamba anatua Jangwani kwa gharama rafiki.

Habari zinasema kwamba Yanga tayari wako kwenye hatua nzuri na anayemsimamia mchezaji huyo ambaye ni mmoja wa viongozi wa kijeshi nchini DR Congo na wanachoendelea kujadiliana kwa sasa ni dau tu ambalo bado limeonekana kuwa kubwa lakini watamalizana ndani ya wiki kadhaa kuanzia sasa.

Eymael amewaambia Yanga kwamba kama ishu hiyo ikishindikana basi warudi kwa Mwendwa ambaye kwa staili ya uchezaji anafiti sana Jangwani kwani ni aina ya kina Saimon Msuva na Mrisho Ngassa ‘wale wenyewe’.

SOMA NA HII  KMC YATUMA SALAMU KWA BIASHARA UNITED

“Huyo kiongozi bado hajatoa jibu kwetu, ila mchezaji mwenyewe (Tuisila) ameshakubali kila kitu, unajua yule ni mchezaji ambaye hauna shaka naye kabisa ngoja tupambane naye. kama tukishindwa ndio tuangalie chaguo la pili,” alisema kiongozi huyo wa Yanga na kuongeza kuwa kocha anazidi kuwapa mapendekezo kila mara na tayari ripoti yake ya awali wanayo ingawa wamemkatalia kumtema Kelvin Yondani ambaye watampa mkataba wa mwaka mmoja.

Yanga mapema msimu uliopita waliwahi kumhitaji Mwendwa lakini ikaelezwa alikubaliana na viongozi aliporudi kwao Kenya akabadilisha gia angani Yanga akitaka fedha zaidi, Kocha Mwinyi Zahera akawaambia viongozi wampige chini.

Lakini kwa sasa tayari Mwendwa ameshapokea simu kutoka Yanga akikubali kila kitu na wamemwambia akaushe kwanza ishu za corona zikiisha aje Dar es Salaam fasta wamalize dili, lakini hapo ni kama mabosi wa Tuisila wataendelea kuzingua.

Kocha Eymael bado amekuwa mgumu kutaja majina lakini ameisisitiza Mwanaspoti kwamba Yanga ijayo itakuwa na mabadiliko makubwa sana, kauli aliyowahi pia kuisema Mwenyekiti msomi, Mshindo Msolla wiki chache zilizopita. GSM waliporejea Yanga.