Home Uncategorized RUVU SHOOTING YAPANIA KUSUKA KIKOSI CHA MAANGAMIZI

RUVU SHOOTING YAPANIA KUSUKA KIKOSI CHA MAANGAMIZI

OFISA Habari wa kikosi cha Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kuwa kwa sasa wanajipanga kusuka upya kikosi cha maangamizi msimu ujao ili wafikie malengo.

Ruvu Shooting msimu wa mwaka 2018/19 walikuwa kwenye hatihati ya kushuka daraja kutokana na kuwa na mwenendo mbovu hali iliyowafanya washtuke mapema kabla ya msimu mpya kuanza.

“Tulipambana kiasi cha kutosha msimu huu ila haikuwa bahati yetu kuwa ndani ya timu zilizomaliza kwenye kumi bora, kwa sasa tunajipanga upya ili kufanya vizuri msimu mpya,” amesema Bwire.

Ruvu imemaliza ligi ikiwa nafasi ya 15 baada ya kucheza michezo 38 imejikusanyia pointi 45.

SOMA NA HII  SIMBA HUYU NI MTU SIO MALAIKA.... MSIJIJAZE UPEPO