Home Uncategorized KIUNGO MUANGOLA RASMI ATUA BONGO KUMALIZANA NA YANGA

KIUNGO MUANGOLA RASMI ATUA BONGO KUMALIZANA NA YANGA

 

KIUNGO, nyota kutoka Angola, Carlos Stenio Fernandes Guimaraes do Carmo Carlinhos, leo Agosti 25 ametia timu Bongo kwa ajili ya kumalizana na mabosi wa Yanga.


Kiungo huyo mwenye uwezo wa kufunga na kutengeneza nafasi za mabao inaelezwa kuwa tayari alikubali kusaaini dili la miaka miwili hivyo leo amekuja kukamilisha kazi pale walipoishia.

 Yanga tayari wameshaanza mazoezi ikiwa ni maandalizi ya kuelekea wiki ya Wananchi inayotarajiwa kuwa Agosti 30 ambayo malengo makubwa ni kuwatambulisha nyota wake wapya na wale ambao walikuwa na kikosi msimu uliopita.

Carlos Fernandes, Kiungo huyo alikuwa anakipiga ndani ya Klabu ya Petro de Luanda ya nchini Angola alitupia jumla ya mabao tisa na kutoa pasi tano za mabao.

SOMA NA HII  SIMBA YALIPIGIA HESABU KOMBE LA FA, KIKOSI CHATIA TIMU SUMBAWANGA LEO