Home Habari za michezo TRY AGAIN ASHUSHA NONDO ZA MAANA SIMBA…ATANGAZA KURUDI KWA MO DEWJI…AMNYOOSHEA KIDOLE...

TRY AGAIN ASHUSHA NONDO ZA MAANA SIMBA…ATANGAZA KURUDI KWA MO DEWJI…AMNYOOSHEA KIDOLE MANARA…


MASHABIKI wa Simba, watembee kifua mbele tajiri wao amerejea kazini kusajili kikosi kazi cha kunyakua ubingwa msimu ujao (2022/23).

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ amezungumza leo na Azam Tv kwamba, rais wa heshima wa timu hiyo, Mohammed Dewji ‘MO’ anarudi kusajili.

Try Again alisema tayari wamefanya kikao na rais wa heshima wa Simba, Mohammed Dewji ‘MO’ watasajili kwa kishindo ili msimu ujao wafanye maajabu.

“Tumeshindwa kufanya vizuri msimu huu hilo halitutoi mchezoni tumekutana kama viongozi klwa lengo la kusawazisha makosa yetu hilo limefanyika kwa usahihi sasa tunafanya mchakato wa kupitia CV za makaocha waliotuma maombi,” alisema na kuongeza;

“Baada ya kupata atakaekuwa sahihi nafikiri kabla ya msimu huu haujaisha atapewa nafasi ya kutoa mapendekezo ya usajili na tutaanza bira kuchelewa ili tuendane na mbio za maandalizi mazuri ya mwanzo wa msimu ‘Pre Season’,”

Wakati huo huo Try Again alitaja sababu zilizomuondoa Pablo Franco kuwa ni kushindwa kufikia malengo ya klabu hiyo ambayo yalikuwa kama sehemu ya makubaliano.

“Pablo ndani ya mkataba wake makubaliano yalikuwa ni kutwaa taji la Ligi, Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) na kuifikisha Simba hatua ya nusu fainali Ligi ya Mabingwa Afrika ameshindwa kufanya hivyo,” alisema na kuongeza;

“Kashindwa kufikia malengo kwa upande wetu tumegundua kuwa pia sio mzoefu na soka la Afrika tumefanya makubaliano ya kuachana naye na alikuwa na ofa hatukuona sababu za kumbakiza tumeachana vizuri na tumemtakia kila la kheri,” alisema.

Wakati huohuo aliwataka wasemaji wa timu pinzani Ligi Kuu Simba na Yanga kutumia nafasi walizonazo kuwaunganisha watanzania na sio kuwasambaratisha huku akiwataka kuzisemea mazuri klabu zao.

“Haji Manara na Ahmed Ally ni wadogo zangu nafurahia wanachokifanya kwenye klabu zao natamani kuona wao ndio wanawaunganisha watanzania kwa kuwaaminisha kuwa mpira sio uadui ni burudani,” alisema.

SOMA NA HII  AUCHO APIGIWA SALUTI NA MWAMBA HUYU