Home Habari za michezo VIONGOZI WA YANGA WATANGAZA KUFANYA KUFURU HII

VIONGOZI WA YANGA WATANGAZA KUFANYA KUFURU HII

Habari za Yanga leo

Uongozi wa Young Africans umeweka wazi kuwa kwa sasa unataka kufanya kufuru ya kwenda anga za vigogo kama Pyramid na Al Ahly kwa kumwaga mabilioni kuhakikisha wanaandika Rekodi ya kufika mbali katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Uongozi wa Young Africans umeahidi kuendelea kumwaga pesa za maana kwa ajili ya kuhakikisha kuwa timu hiyo inafanya vyema, katika michuano ya Kimataifa ambapo timu hiyo inaendelea kushiriki.

Aidha uongozi wa Young Africans umeweka wazi kuwa msimu uliopita katika michuano ya kimataifa walifanikiwa kutumia zaidi ya shilingi Bilioni 1.2 katika kumwaga posho kwa ajili ya wachezaji katika michuano ya Kimataifa.

Msimu uliopita ikumbukwe Young Africans walitinga fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika ambapo walipoteza dhidi ya USM Algers katika mchezo wa fainali, lakini pia walianzia katika ligi ya mabingwa Barani Afrika na kutolewa katika hatua ya pili dhidi ya Al Hilal.

Ofisa Habari wa Young Africans, Ally Kamwe amesema: “Msimu uliopita Young Africans ilitumia zaidi ya shilingi Bilioni 1.2 kwa ajili ya posho za wachezaji katika michuano ya kimataifa na msimu huu pia zitatumika pesa nyingi.

“Malengo ni kuhakikisha kuwa tunafanya vyema katika michuano hii ya kimataifa ili tuweze kufika mbali, malengo yetu ni kufika hatua ya makundi na lazima wachezaji wapewe posho nzuri katika kila hatua ambayo wataweza kuvuka, huo umekuwa ni utamaduni wetu.

“Timu kubwa kama Pyramids na zingine hutumia pesa nyingi sana kwa kuwa wanao msuli mkubwa wa pesa hivyo na sisi ni wakati wetu wa kuhakikisha kuwa tunatumnia mbinu nzuri za kufanya vyema zaidi,” alisema kiongozi huyo.”

SOMA NA HII  WACHEZAJI HAWA WALIOACHWA NA SIMBA, YANGA WAPATA MAJANGA KATIKA USAJILI