Home Taifa Stars SERIKALI KUIPIGA TAFU TAIFA STARS

SERIKALI KUIPIGA TAFU TAIFA STARS


 KATIBU Mkuu wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi amesema Serikali imejipanga kuisaidia timu ya taifa ya Tazania, Taifa Stars kwa kuipatia fedha ili kuongeza ufanisi wa timu hiyo ndani na nje ya nchi.

 

Abbasi amesema hayo Mei 3, 2021 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Katibu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Alfred Kidao.


Viongozi hao wamezungumzia namna ya kuiwezesha Stars kwenye maandalizi ya michuano ya awali ya kufunzu Kombe la Dunia yanayotarajiwa kufanyika mwezi Juni hadi Agosti 2021.


 

“Ili kupata matokeo mazuri wachezaji wetu lazima wawe vizuri kifedha hii itawasaidia kisaikolojia kuweza kupata matokeo mazuri.” Amesema Abbasi.

 

Ameongeza kuwa Serikali imejipanga kuanzisha vyanzo mbalimbali vya mapato kwa ajili ya michezo ikiwemo kurudisha mchezo wa Bahati Nasibu (Sport Betting Nationary Lottary).

 

Kwa upande wake Kidao amesema maandalizi yote yamekamilika huku akieleza kuwa changamoto iliyobaki ni ukosefu wa rasilimali fedha ambapo ameshukuru namna Serikali inavyojipanga kukabili changamoto hiyo ikiwemo kusaidia posho za wanamichezo kutolewa mapema.

 

Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Tanzania Yusuph Singo.

SOMA NA HII  KAKOLANYA AFURAHIA KUITWA STARS...KUJIWEKA SAWA MUDA WOTE NI MUHIMU...HATA NIKIKAA BENCHI FRESH TU