Home Simba SC SIMBA YAIWEKA KANDO KAIZER CHIEFS KWA MUDA, HESABU ZAO NI MEO 8

SIMBA YAIWEKA KANDO KAIZER CHIEFS KWA MUDA, HESABU ZAO NI MEO 8


 BEKI kisiki wa kikosi cha Simba, Joash Onyango amesema kuwa kwa sasa hawafikirii mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Kaizer Chiefs badala yake wanazitazama mechi zao zilizo karibu kwa sasa.

Simba ipo hatua ya robo fainali kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na baada ya droo iliyofanyika Aprili 30 imepangwa kukutana na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.

Onyango ambaye ni chaguo la kwanza kwa Kocha Mkuu, Didier Gomes amesema kuwa kwa sasa hawaifikirii mechi hiyo inayotarajiwa kuchezwa kati ya Mei 14-15 na ule wa marudio unatarajiwa kuchezwa kati ya Mei 21-22 Uwanja wa Mkapa.

Onyango amesema:”Bado kwa sasa kuna mechi ambazo zipo mbele yetu kabla ya kukutana na Kaizer Chiefs hivyo hesabu zetu zitakuwa kwenye mechi za karibu ambazo tunahitaji kupata ushindi.

“Kikubwa ni kuona kwamba tunapata matokeo chanya katika mechi ambazo tutacheza na imani yetu ni kwamba tutafanya vizuri, mashabiki watupe sapoti,” .

Mchezo ujao wa Simba ni Mei 8 ambapo itakuwa ni dhidi ya Yanga utakaochezwa Uwanja wa Mkapa.

SOMA NA HII  A-Z JINSI SIMBA 'ILIVYOWASOSOMOLA YANGA' WA IVORY COST ...BANDA, SAKHO WAAANZA KULIPA MSIMBAZI....