Home news BAADA YA KUMALIZANA NA YANGA..TSHISHIMBI AUTAKA URAIA WA TZ AICHEZEE TAIFA STRAS

BAADA YA KUMALIZANA NA YANGA..TSHISHIMBI AUTAKA URAIA WA TZ AICHEZEE TAIFA STRAS


Nahodha wa zamani wa Yanga, Papy Tshishimbi amevutiwa na maisha ya Tanzania na kusema yupo tayari kubadilisha uraia wake ilia pate nafasi ya kuichezea timu ya taifa ya Tanzania “Taifa Stars’.

Tshishimbi raia wa DR Congo alisema iwepo atapata nafasi ya kuitwaa Taifa Stars yupo tayari kubadilisha uraia wake.

Tshishimbi alisema nje na soka anafurahia maisha ya Tanzania namna wanavyopenda soka ikiwa ni sambamba na nchi yenyewe ilivyo na maisha ya kawaida.

“Mbali na soka mimi napenda maisha ya Tanzania pia nafuraishwa na umoja na upendo uliopo kutoka kwa wananchi wa nchi hii hawana ubaguzi wanampenda kila mtu na wanaushirikiano mzuri tofauti na mataifa mengine niliyowahi kucheza,” alisema Tshishimbi.

Tshishimbi aliongeza kuwa mbali na kuwa na mpango wa kufanya hivyo kwa upande wake endapo ataweza kufanikisha hilo basi hadi familia yake itatakiwa pia ufuate uraia wake ili waweze kuishi pamoja Tanzania.”

Tshishimbi kwa sasa ni mchezaji huru, baada ya kumaliza mkataba wake na As Vita ya Congo DRC na sasa yupo hapa nchini kwa mambo yake binafsi.

SOMA NA HII  ILE ISHU YA SIKAONGA KUTUA SIMBA IMEFIKIA HIVYI...RIPOTI YA PABLO YAFICHUA MENGI..BARBARA KAMA KAWA...