Home Habari za michezo SIMBA WAJIBU HOJA ZA DK KIGWANGALA…TRY AGAIN AMSHUKIA JUMLA JUMLA…AMPELEKA BUNGENI KWA...

SIMBA WAJIBU HOJA ZA DK KIGWANGALA…TRY AGAIN AMSHUKIA JUMLA JUMLA…AMPELEKA BUNGENI KWA ‘SHANGAZI’….


Salim Abdallah maarufu ‘Try Again’ Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya Simba ambaye amefunguka mengi juu ya timu hiyo na kwamba itarudi kwenye levo zake kwa kishindo.

Try Again anasema; “Tunarudi kwa kishindo, tunarudi kwa kishindo. Nimezungumza na mwekezaji wetu MO Dewji kuwa atasajili (wachezaji).

“Tutawekeza kwenye miundombinu, kikubwa tunaomba wapenzi wa Simba tumpe ushirikiano, lakini tunawaahidi tutarudi kwa kishindo.

“Sasa ni wakati wa kufanya mabadiliko ya kikosi, tunasajili vizuri, tutabaki na wachezaji wazuri, kuna wengine umri umekwenda na viwango vimeshuka, lakini hatutawaacha vibaya…Tunawashukuru sana wachezaji na benchi la ufundi.

“Nawashauri viongozi wenzangu, ni vizuri kushauri, lakini tutumie njia bora. Kwa nini tulipofanya vizuri nyuma hawakusema? Haipendezi wajumbe wa bodi wana nafasi ya kushauri ndani, lakini wanatoka wanakwenda kuzungumza huko nje. Si jambo jema.

“Tumemsikia Dk Hamis Kigwangalla. Tumepokea ushauri wake, lakini ni vizuri kusema mapema, kwa nini anasubiri kusema? Pale bungeni kuna Rashid Shangazi ni mjumbe wa bodi angeweza kuwasilisha ushauri wake.”

SOMA NA HII  KISA AL AHLY....SIMBA NA YANGA KUUNGANA KWA MUDA...CAF WATOA BARAKA ZAO...