Home Habari za michezo BAADA YA KUMALIZANA NA NTIBAZONKIZA….SINGIDA BIG STARS YASHUSHA KIFAA HIKI KINGINE…MAKAMBO NAYE...

BAADA YA KUMALIZANA NA NTIBAZONKIZA….SINGIDA BIG STARS YASHUSHA KIFAA HIKI KINGINE…MAKAMBO NAYE NDANI…


SINGIDA Big Stars kweli wameamua, kwani baada ya kuanza kuwavuta mafundi kadhaa wa soka waliokuwa Simba na Yanga, kwa sasa wamemgeukia straika wa Mbeya Kwanza, Habib Kiyombo ili kuwa sehemu ya kikosi chao kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Timu hiyo iliyopanda daraja kutoka Ligi ya Championship, imenasa saini ya nyota huyo wa zamani wa Mbao na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya klabu hiyo kililiambia Mwanaspoti tayari wamemalizana na Kyombo kwa mkataba wa miaka miwili ili kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho.

“Usajili bado unaendelea mambo yakiwa tayari utambulisho utaanza kwa mchezaji mmoja mmoja tunahitaji kikosi cha ushindani tumetoka kwenye ligi ngumu Championship tumefanya vizuri hatutaki kuanza kwa aibu,” alisema na kuongeza;

“Tunatambua utofauti uliopo Championship na Ligi Kuu ndio maana tumeanza usajili mapema kwa kuchanganya wachezaji wazoefu na damu changa tunatarajia mambo makubwa kutokana na usajili huu.”

Mbali na huyo wachezaji wengine waliomalizana nao ni Deus Kaseke, Abdulmajid Mangalo, Paul Godfrey ‘Boxer’, Victor Akpan, Gadiel Michael na Aziz Andambwile huku wengine wakitajwa kama Saido Ntibazonkiza na Heritier Maka mbo kuwa miongoni mwa watakaoitumikia timu hiyo.

SOMA NA HII  WAKATI SAKHO AKIZIDI KUKIWASHA SIMBA...NKANE APATA 'PANCHA' YANGA...UONGOZI WAJA NA HOJA HIZI...