Home Uncategorized KOCHA YANGA:HARUNA NIYONZIMA HANA NIDHAMU

KOCHA YANGA:HARUNA NIYONZIMA HANA NIDHAMU

 


MUDA mfupi kabla ya kusitishiwa mkataba wake ndani ya Yanga, Oktoba 3, aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Zlatko Krmpotic alisema kuwa sababu kubwa iliyomfanya asimtumie mchezaji Haruna Niyonzima kikosi cha kwanza ni utomvu wa nidhamu.

Krmpotic  alikiongoza kikosi cha Yanga kwenye mechi tano za Ligi Kuu Bara ambazo ni dakika 450 na alishinda mechi nne huku akilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Tanzania Prisons, Uwanja wa Mkapa.

Kwenye mechi tano za ligi ambazo Krmpotic alikuwa kwenye benchi, Niyonzima alianza kikosi cha kwanza mechi moja mbele ya Mbeya City na alitumia dakika 69,mechi mbili hakucheza mbele ya Tanzania Prisons na Mtibwa Sugar .

Mechi mbili alianzia benchi ilikuwa mbele ya Kagera Sugar alitumia dakika 7 na mbele ya Coastal Union alitumia dakika 45, jumla Niyonzima ametumia dakika 121 kati ya 450 akikosekana kwenye dakika 329.

Krmpotic alisema:”Haruna Niyonzima ni mchezaji mzuri ila ana mambo yake ambayo yalikuwa ni nje ya uwanja, mfano kabla ya mechi yetu dhidi ya Coastal Union kuna siku mbili alichelewa kurudi kambini ikiwa ni pamoja na Jumatatu, sasa hapo ilikuwa ngumu kumuanzisha moja kwa moja kikosi cha kwanza.”


SOMA NA HII  BAADA YA KUITUNGUA YANGA, MTIBWA SUGAR YAIPIGA MKWARA MZITO SIMBA