Home news RUVU SHOOTING : TUTAIFUNGA NAMUNGO

RUVU SHOOTING : TUTAIFUNGA NAMUNGO


 OFISA Habari wa Ruvu ShootingMasau Bwireamefunguka kuwa, wamejipanga kuchukua pointi tatu dhidi ya Namungo FC katika mchezo wao unaotarajiwa kupigwa Julai 15, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mabatini, Pwani.

 

Ikiwa nafasi ya 10 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, Ruvu Shooting imekusanya pointi 38 katika michezo 32, huku ikishinda 10, imepoteza 14 na sare nane.

 

Bwire amesema maandalizi ya mechi zao mbili zilizosalia yanaendelea vizuri, lakini wamejikita zaidi katika mechi ijayo dhidi ya Namungo.

 

“Maandalizi yanaendelea kama kawaida na tupo tayari kwa mechi muda wowote, tumejipanga kuhakikisha hachomoki mtu katika mechi hizo lazima tuchukue pointi zote dhidi ya wapinzani wetu.

 

“Tunafahamu hakuna mechi rahisi kwenye soka, hivyo ni wazi huu mchezo utakuwa mgumu kwa sababu kila mtu anataka hizo pointi ili iweze kuwa salama kwa upande wake, lakini na sisi kwa upande wetu tumejipanga vizuri sana,” amesema Bwire.

 

Ruvu Shooting haina uhakika wa kubaki ndani ya ligi ikiwa itayeyusha pointi zake sita kwenye mechi mbili zilizobaki hivyo ina kazi ya kufanya ili kupata matokeo.


Pointi zake zinaweza kufikiwa na Coastal Union iliyo nafasi ya 17 na pointi 34 baada ya kucheza mechi 32.


Baada ya mchezo huo, Julai 18, mwaka huu, Ruvu Shooting itamaliza msimu uwanja wa nyumbani kwa kucheza dhidi ya Azam.

SOMA NA HII  MAMBO HADHARANI FAILI LA AFYA YA KRAMO HILI HAPA