Home CAF SIMBA YAFANYA MAAJABU YAKE…KLABU BINGWA MIDOMO WAZI…RAJA CA HAWAAMINI MACHO YAO

SIMBA YAFANYA MAAJABU YAKE…KLABU BINGWA MIDOMO WAZI…RAJA CA HAWAAMINI MACHO YAO

Habari za Simba SC

LICHA ya Simba kutofanya vizuri kwenye mechi mbili za Klabu Bingwa Barani Afrika lakini ndio timu pekee iliyopiga hesabu zake vizuri kwenye mechi muhimu zilizompatia alama sita na kumuweka nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi C.

Simba ipo kwenye Kundi C ikiwa na pointi sita nyuma ya Raja Casablanca ya Moroco ambayo ina pointi 12 na nyuma yake ipo Horoya yenye pointi nne.

Maajabu ya Simba ni kwamba kwenye kundi lake inashika nafasi ya pili ikiwa na alama sita na mabao mawili pekee ambayo kwa tafsiri ya kawaida ni timu iliyofunga mabao mawili na kufungwa mabao 4 ikiwa na negativu mbili lakini bado iko nafasi ya pili.

Ukiangalia kwenye Kundi D ambalo linaongozwa na Esperance Tunis na alama 9, huku Zamalek ikiwa na alama 4 na mabao 3 ambaye anatofautiana alama 2 na Simba na bao moja akimpita lakini bado anashika nafasi ya tatu.

Mabingwa wa kihistoria nchini Misri, Al Ahly ambayo ni tishio kwa barani Afrika ipo nafasi ya tatu ikiwa na alama nne na mabao 7, ukitazama na ukubwa alionao lakini bado inashika nafasi hiyo licha ya kufunga mabao mengi juu ya Al Hilal ambayo inashika nafasi ya pili na alama 9.

Kwenye mechi nne ilizocheza Simba imeshinda mbili ambazo moja ugenini bao 1-0 na Vipers na nyingine ilishinda katika Uwanja wa Benjamin Mkapa na timu hiyo hiyo kwenye mechi ya marudiano bao 1-0.

SOMA NA HII  HATIMAYE WAPINZANI WA SIMBA...KLABU BINGWA...WAANZA SAFARI KUTUA DAR