Home Habari za michezo ALLY KAMWE :- TUMESHTUSHWA NA PROPAGANDA ZA SIMBA…KESHO WATAONA UBOVU WETU…

ALLY KAMWE :- TUMESHTUSHWA NA PROPAGANDA ZA SIMBA…KESHO WATAONA UBOVU WETU…

Habari za Michezo leo

Afisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa siku ya Jumapili watakwenda kuwaonesha watani Simba kuwa wao sio wabovu kisa kufungwa na Al Hilal FC kunako Ligi ya Mabingwa Afrika.

”Tunakwenda kuwajibu Simba kwa vitendo, tumeshtushwa na propaganda za kusema kuwa Yanga ni mbovu. Sisi Klabu Bingwa Afrika tulishindwa kutimiza malengo yetu lakini haimaanishi sisi sio bora.”

Yanga inajipanga kukabiliana na Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaopigwa siku ya Jumapili katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

SOMA NA HII  ZIKIWA ZIMESALIA SIKUU CHACHE LIGI KURUDI TENA...'PRINCE DUBE' KAIBUKA NA HILI KWA YANGA...ADAI YUKO TAYARI...