DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa walistahili kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa kuwa ulikuwa ni mpango wao tangu awali.
Ushindi wa jana mbele ya Coastal Union wa mabao 2-0 uliwafanya wafikishe jumla ya pointi 79 ambazo hazitafikiwa na timu yoyote kwa sasa hivyo walitangazwa kuwa mabingwa wa msimu wa 2020/21 wakiwa na mechi mbili mkononi.