Home Uncategorized SIMBA WATIA TIMU TANGA, ALHAMISI KUVAANA NA COASTAL UNION

SIMBA WATIA TIMU TANGA, ALHAMISI KUVAANA NA COASTAL UNION


KIKOSI cha Simba kimewasili salama leo Julai 21 Tanga ambapo kimekwenda kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union unaotarajiwa kuchezwa Julai 23.

Uongozi wa Simba umesema kuwa unahitaji pointi tatu muhimu ili kuwa mwendelezo kuelekea mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Namungo FC. 

Mchezo wa fainali unatarajiwa kuchezwa Agosti 2, Uwanja wa Nelson Mandela,  Sumbawanga. 

Patrick Rweyemamu,  meneja  wa Simba amesema wana matumaini ya kupata ushindi mbele ya Coastal Union kwa kuwa wapo tayari.

“Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Coastal Union,  utakuwa mchezo mgumu kwetu lakini ni hesabu za kuelekea kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho. 

“Wachezaji wapo tayari na morali ni kubwa kwa kuwa ni kazi yao hivyo mashabiki wajitokeze kutupa sapoti kwenye mchezo wetu,” amesema. 

Simba ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 84, inakutana na Coastal Union ambayo ipo nafasi ya sita na pointi 52.

SOMA NA HII  MABINGWA WA AFRIKA ALGERIA WANATISHA KINOMA